- Serikali imeanzisha uchunguzi kuhusu uapishaji wa Raila Odinga
- Waziri Fred Matiang'i anasema shughuli hiyo ililenga kuangusha serikali iliyopo sasa
- Hatua mwafaka kisheria zitachukuliwa pindi uchunguzi utakapokamilika
Utawala wa Jubilee wa Rais Uhuru Kenyatta umeanzisha uchunguzi dhidi ya uapishaji tatanishi wa kiongozi wa National Super Alliance (NASA) Raila Odinga mnamo Ijumaa,Januari 30, katika bustani ya Uhuru Park.
Waziri Fred Matiang'i mnamo Ijumaa, Januari 31, alisema shughuli hiyo haramu ilidhamiria kuangusha serikali iliyopo.
Matiang'i vilevile alisema hatua itachukuliwa dhidi Raila Odinga, na waandalizi wa hafla hiyo pindi uchunguzi utakapokamilika.
Habari Nyingine: Hatimaye Raila ala kiapo kuwa 'rais' wa wananchi

Habari Nyingine: Uhuru anafaa kumkamata Raila Odinga na kumshtaki - Mutahi Ngunyi
Kilichoshuhudiwa Uhuru Park lilikuwa jaribio lililopangwa vyema la kupindua na kuangusha serikali iliyoidhinishwa kisheria ya Jamhuri ya Kenya," Matiang'i alisema.
"Serikali imeanzisha uchunguzi kamili kuhusu ‘uapishaji’ wa Raila Odinga. Uchunguzi huo utahusisha washiriki wenza na wahisani.” Matiang'i alisema.
Habari Nyingine: Wakenya wamdhihaki Raila baada ya kiapo chake cha mtu mmoja

Jinsi ilivyoripotiwa na TUKO.co.ke, Raila aliapishwa kama rais wa wananchi katika hafla iliyosusiwa na naibu wake Kalonzo Musyoka na vinara wenzake wa NASA Moses Wetangula na Musalia Mudavadi

Ususiaji huo ulivutia shutuma tele kutoka kwa wafuasi wa NASA na kuwalazimu watatu hao kudai walikuwa wamezuiliwa na polisi huku Raila akitoweka.
Serikali ilikuwa imeharamisha uapishaji huo ikisema ulikuwa kinyume na sheria.
Vyombo vya habari pia vilifungwa kwa lazima kuzuia upeperushaji wa hafla hiyo iliyofanyika Uhuru Park.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una taarifa ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4F4f5ZmrJqomai1orbIZq6aZaKWtq2tjK6joqOlrK5utsCroJuhn2K5onnKrqeippSqrm6%2FxKugpJmcnnqiv8SmmGavka%2B2s7WMppitoZGjtKp6x62kpQ%3D%3D