-Baadhi ya wezi hao hujifanya kama wateja na kuwatambua wateja waliotoa pesa nyingi kwenye benki
-Wizi huo unawahusiha wafanyikazi wa benki, polisi na majambazi
-Ripoti zinaarifu kuwa wateja wote walioripoti visa hivyo walishambuliwa na kuibiwa pesa baasa ya kuondoka kwenye benki
Ripoti za hivi punde za wateja kuibiwa pesa wanapoondoka kwenye benki zimewapa wateja wengi wasiwasi, licha ya kuwa wengi walikuwa wakiamini benki kuwa eneo salama.
Baadhi ya majambazi wanaoendeleza wizi huo hujifanya kuwa wateja na kuwatambua wateja aliotoa fedha nyingi kisha kuwaandama wanapotoka nje ya benki.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine: Susan Kaittany azungumzia chuki ilioko kati yake na Betty Kyalo

Habari Nyingine: Otile Brown na Vera Sidika watoka nje pamoja kwa mara ya kwanza na inafurahisha
Kwa miezi miwili iliyopita, visa vya watu kuvamiwa na kuibiwa hela baada ya kuondoka kwenye benki vimeripotiwa katika maeneo ya Machakos, Kitui na Makueni.
Kwenye tukio la hivi punde la Jumapili, Aprili 29 mjini Machakos, ilidaiwa kuwa maafisa wa polisi walihusika, tukio ambalo limepingwa na kamanda wa polisi eneo hilo.
Aprili 9, John Bosco ambaye ni mwalimu katika shule ya upili ya Thavu alitoa KSh 430,000 kutoka kwenye benki ya KCB eneo la Wote na kupanda matatu iliyokuwa ikielekea Kathonzweni.
Aliposhuka kwenye stani ya basi ya Kathonzweni, alikabiliwa na watu wanne waliojitambulisha kama maafisa wa polisi.
Habari Nyingine: Lilian Muli hatimaye azungumzia uvumi kuwa alipachikwa mimba na Jeff Koinange

Alifungwa kwa pingu na kuwekwa kwenye gari aina ya Fielder akipelekwa mjini Wote.
Walimsukuma nje ya gari, tukio lililomwacha na majeraha ya kichwa na mikono.
Alikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Makueni na kulazwa.
Gari lililotumiwa lenye nambari ya usajili KCJ 642R lilipatikana limeachwa kando ya barabara ya Wote kuelekea Kako.
Polisi waliokuwa wakichunguza tukio hilo walipata kuwa walipata nambari za usajili KCL 590B NA KCM 733J kwenye gari hilo.
Kwenye tukio lingine mwezi Machi eneo la Kitui, inadhaniwa kuwa wafanyikazi au majambazi waliokuwa wakijifanya kuwa ni wateja ndani ya benki moja walimtambua mfanyibiashara mmoja na kumuibia pesa alipotoka ndani ya benki.
Habari Nyingine: Kundi la wasichana hatari wahangaisha wanawake Mombasa, wawanyang'anya waume wao
Genge hilo lililojitambulisha kama maafisa wa polisi lilimvamia kati ya ofisi za bodi ya kitaifa ya nafaka na mazao (NCPB) na benki hiyo.
Morris Nkanata alikwenda kwenye benki ya KCB tawi la Kitui na kutoa KSh 650,000.
Alipoondoka kwenye benki, alizuiwa na gari aina ya Toyota NZE iliyokuwa na watu wanne.
Walimwonyesha kilichoonekana kama kitambulisho cha afisa wa polisi wa utawala (AP) kabla ya kumlazimisha kuingia kwenye kiti cha nyuma.
Walichukua simu yake na kumfunga kwa pingu.
Genge hilo lilimwacha Nkanata eneo la Kanyonyo baada ya kuchukua pesa alizokuwa nazo na kumlazimisha kutoa KSh 140,000 alizokuwa nazo kwenye akaunti ya benki kwa kutumia simu.
OCPD wa eneo la Kitui ya Kati alisema kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
Taarifa ya Lucky Omenda – Ripota, Nairobi
Read ENGLISH VERSION
Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News
Familia 4 za kutia moyo na kupendeza zaidi za wanasiasa wa Kenya wenye ushawishi | TUKO TV
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibH92hZFmrpqekaPGqrfAs6Bmr5Fir6a6yqJkp5ldpbyttdKiZLCZnpbAqbXRoqKimZ6WeqzB1pqgm6GRYsSiwMSjmGavkaOusMDOmmSpnaOWeq%2FFyKeeomaYqbqt